Home KITAIFA USHINDI WA MECHI YA CHAN, STARS YAVUNA MILIONI 60

USHINDI WA MECHI YA CHAN, STARS YAVUNA MILIONI 60

100
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekabidhi Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) kitita cha shilingi milioni 20 (Goli la Mama) baada ya kuifunga Burkina Faso 2 – 0 katika ufunguzi wa Mashindano ya CHAN Agosti 2, 2024 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ambazo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kama alivyoahidi kila goli moja shilingi milioni kumi.

Pia Prof. Kabudi nae ametoa shilingi milioni 20 pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndg. Chalamila ambaye amewapatia kiasi cha Milioni 20.

Kwa ujumla Taifa Stars imevuna Milioni 60 baada ya ushindi wa jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here