Beki wa kimataifa wa Mauritania, Khadim Diaw (27), amekuwa lulu sokoni mwezi huu wa Januari 2026 baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Al Hilal Omdurman kutokana na madai ya kutolipwa mishahara kwa miezi kadhaa.
Hivi sasa, beki huyo mzoefu yuko kwenye mazungumzo ya kina na miamba kadhaa ya soka barani Afrika, ikiwemo Simba SC ya Tanzania, pamoja na klabu za Algeria za MC Alger na JS Kabylie ambayo inatajwa kumpa ofa ya mkataba wa miaka mitatu ili kuimarisha safu yao ya ulinzi.
Licha ya Simba SC {@simbasctanzania} kuonyesha nia ya dhati ya kumnasa Diaw kwa ajili ya mashindano ya kimataifa, ushindani umekuwa mkubwa kutoka kwa JS Kabylie ambao tayari wamefikia makubaliano ya awali na mchezaji huyo kufuatia kushinda kesi yake ya kimkataba dhidi ya Al Hilal mbele ya FIFA.
Diaw anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuzuia na kupandisha mashambulizi kupitia pembeni (overlapping), sifa ambazo zimemfanya kuwindwa pia na Raja Casablanca na ES Sétif kuelekea mzunguko wa pili wa msimu huu.










Leave a Reply