INAELEZWA kuwa Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Fadlu Davids kwenye mechi za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25 yupo kwenye rada za mabosi wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Ahoua ni anayevaa jezi namba 10 mgongoni ana uwezo kwenye kufunga na kutoa pasi za mabao akiingia kwenye orodha ya wakali wa mapigo huru ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
Katika mabao 15 aliyofunga mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akiwa kafunga mabao 14 na kwa pigo la kichwa alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya Ellie Mpanzu.
Kwenye mchezo huo Ahoua alifunga hat trick yake ya kwanza akiwa na uzi wa Simba SC ambapo alichaguliwa kuwa mchezaji bora Simba SC iliposepa na pointi tatu mazima katika mchezo wa ligi.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wanamfuatilia kwa ukaribu kiungo huyo ambaye amehusika katika mabao 23 ndani ya ligi namba nne kwa ubora kati ya 63 yaliyofungwa na timu hiyo kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika.