Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » YANGA YAIJIBU TFF, DAWA YA DENI NI KULIPA KWA WAKATI
    KITAIFA

    YANGA YAIJIBU TFF, DAWA YA DENI NI KULIPA KWA WAKATI

    ChikaoBy ChikaoJune 11, 202512 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    yanga
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    Klabu ya Yanga imejibu mapigo baada ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kudai klabu hiyo fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kuilipa kwa TFF huku ikidai kuwa haijawahi kulipwa fedha yoyote ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa Misimu mitatu mfululizo, (2021/2022, 2022/2023 na 2023/24).

    Taarifa ya Juni 10, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza taarifa ya TFF Madai hayo imeshindwa kufafanua deni lenyewe na kubainisha kuwa TFF wamekuwa wakishikila fedha hizi za Ubingwa kwenye akaunti zao kila Msimu unapomalizika huku wakifahamu ni makosa na ni kinyume cha utaratibu.

    Yanga Sc imesema hakuna uthibitisho wowote wa kimaandishi kuonyesha kama TFF wamewahi kulipa fedha hizo za Ubingwa kwa Klabu ya Yanga na na kusisitiza kuwa ni aibu na fedheha na kumtia dosari mdhamini kuendesha mashindano bila kumlipa Bingwa kwa misimu mitatu mfululizo.

    “Tunaelekeza, dawa ya deni ni kulipa kwa wakati ikiwa ni haki ya mshindi na inampa heshima mdhamini wa mashindano. leleweke, ada za malipo ya wachezaji wa kiger kigeni walizozisema kwenye taarifa yao hulipwa mwanzo wa msimu mpya na hela hizi za Ubingwa hutolewa Mwisho wa msimu.” — imesema taarifa ya Yanga Sc.

    “Klabu ya Young Africans haijawahi kupokea taarifa yoyote rasmi kutoka TFF kuhusu Klabu yetu kuwa na deni kwao. Uongozi wa Klabu ya Young Africans unaendelea kusisitiza kulipwa pesa yake ya Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, kwa msimu wa 2023/24 ili tuweze kucheza mchezo wa Fainali siku ya tarehe 28 Juni, 2025.” — imesema Yanga Sc

    Yanga SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleBAADA YA KUONA FEI TOTO ANAWEZA KUSEPA…AZAM WAHAMISHA NGUVU KWA STAA WA SIMBA
    Next Article TFF YATANGAZA UCHAGUZI MKUU AGOSTI 16, 2025 JIJINI TANGA

    Related Posts

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    April 26, 2026

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    April 26, 2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    April 25, 2026
    View 1 Comment

    1 Comment

    1. muppu on June 12, 2025 8:29 am

      Pretty! This has been a really wonderful post. Many thanks for providing these details.

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    YANGA, AZAM FC USO KWA USO KUSAKA FAINALI YA MUUNGANO

    SIMBA YASHIKA NAFASI YA 19 DUNIANI, IPO LEVO ZA MADRID

    HILI HAPA DAU LA KUMPATA COLE PALMER

    TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI TAREHE 25.4.2025

    PRESHA YA KUUKOSA UBINGWA YATAWALA REAL MADRID

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.