Mshambuliaji wa klabu ya Pyramids ya Misri Fiston Kalala Mayele jana ametwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa Ligi kuu soka ya Misri.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Congo DR ametwaa tuzo hiyo baada ya kucheza michezo 23 na kufunga magoli 8 huku akipika magoli mawili.
Kwenye msimu huo pia Mayele alifunga magoli 6 kwenye mechi 10 za Ligi ya Mabingwa Afrika yaliyosaidia Pyramids kuwa Mabingwa Afrika.