Author: Chikao

Wakati Yanga ikitangaza kuachana na Miguel Gamondi na msaidizi wake Moussa Ndaw leo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limempa adhabu ya kifungo cha mechi tatu na faini ya Sh 2 milioni kutokana na utovu wa nidhamu. Taarifa iliyotolewa na mtendaji mkuu wa Yanga leo, imeeleza kuwa Gamondi amevunjiwa mkataba wake kama ilivyo kwa Ndaw. Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza sababu za kuachana na Gamondi lakini habari za uhakika ni kuwa sababu ni mwenendo usioridhisha wa timu hiyo msimu huu. Inaonekana kutokuwa siku nzuri kwa Gamondi kwani kuwekwa kando kwake kumetangazwa katika siku ambayo kamati ya usimamizi na uendeshaji…

Read More

Ligi karibia zote barani ulaya leo kutakua na michezo mikali ambayo inaweza kukupatia mkwanja wa kutosha, Kwani mabingwa wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet wanamwaga Odds pale kwenye tovuti yao. Kuanzia pale kwenye ligi pendwa kabisa duniani ligi ya Uingereza itapigwa michezo mikali, Ligi kuu ya Hispania La Liga, nchini Italia Serie A, ligi kuu ya Ujerumani Bundeliga, pamoja na ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 ligi zote hizi zinaweza kufanya ukanyakua mkwanja mrefu. EPL Kunako ligi kuu ya Uingereza leo kutakua michezo kadhaa mikali lakini mchezo ambao utatolewa macho zaidi ni mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal, Mchezo ambao umepewa Odds…

Read More

UEFA Yatoa Ufafanuzi kuhusu Sakata la Vinicius Jr Kukosa Ballon d’Or Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) limejitokeza kueleza msimamo wake kuhusu sakata linalomhusu mchezaji nyota wa Real Madrid, Vinicius Jr, ambaye alikosa tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu. UEFA imekemea vikali uvumi unaoenea kuhusu suala hilo, na kutishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote anayesambaza taarifa zisizo sahihi zinazomhusisha Rais wake, Aleksander Ceferin, na maafisa wengine. Sakata la Kukosa Ballon d’Or Kabla ya hafla ya utoaji tuzo ya Ballon d’Or jijini Paris, Ufaransa, kulikuwapo na matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka kwamba Vinicius Jr angeweza…

Read More

BODI ya Ligi Tanzania (TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ambapo mchezo wa Ligi Kuu namba 82 kati ya Simba Sc dhidi ya KMC Fc uliokuwa uchezwe Jumanne Novemba 5, 2024 katika dimba la KMC Complex sasa utapigwa siku ya Jumatano, Novemba 6, 2024 katika dimba hilo hilo. Aidha TPLB imefanya mabadiliko mengine ambapo mchezo namba 89 wa Simba Sc dhidi ya Pamba Jiji ambao ulipangwa upigwe Novemba 21 sasa utapangiwa tarehe nyingine.

Read More

Yanga Princess imepeleka malalamiko Shirikisho la Soka (TFF) baada ya kugundua Alliance Girls imemtumia mchezaji wa kigeni kinyume na sheria. Oktoba 12 Uwanja wa Nyamagana zilikutana timu hizo kwenye mchezo wa raundi ya pili ya wanawake na mechi ikitamatika wa sare ya bila kufungana. Baada ya Yanga kugundua kuwa timu hiyo ilifanya udanganyifu kwa kumtumia mchezaji huyo ilipeleka malalamiko kwa TFF. Alipotafutwa Mratibu wa Yanga, Kibwana Matokeo juu ya sakata hilo alisema, “ni kweli tumepeleka malalamiko.” Huku akikataa kufafanua jambo hilo. Kwa upande wake Mwenyeiti wa Akademi ya Alliance, Nyaitati Stephano alisema hawajapokea barua yoyote kutoka TFF. Mwenyekiti wa Chama…

Read More