KHALID Aucho kiungo mkabaji wa Yanga SC huenda akaongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Jangwani.
Yanga SC ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25 na miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye kikosi cha kwanza ni Aucho.
Baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700, Aucho alicheza mechi 22 akikomba dakika 1,735. Katika mabao 83 yaliyofungwa na Yanga SC kwenye ligi alihusika kwenye mabao mawili, alifunga moja na kutoa pasi moja ya bao.
Mkataba wa Aucho umegota mwisho baada ya msimu kukamilika. Taarifa zinaeleza kuwa huenda akaongeza mkataba wa mwaka mmoja kusalia ndani ya Yanga SC msimu wa 2025/26.
Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo na Aucho na Yanga SC yamefikia sehemu nzuri na ataongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwa katika kikosi hicho chenye jumla ya mataji 31 ya ligi.