Home KITAIFA YANGA YAIANZA SAFARI YA ANGOLA BAADA YA KUMCHAPA MTANI

YANGA YAIANZA SAFARI YA ANGOLA BAADA YA KUMCHAPA MTANI

295
0
Kikosi Kamili cha Yanga 2025/26

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Romain Folz, wameondoka nchini kuelekea Angola kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 16, 2025 majira ya saa 11:00 jioni, Yanga SC walifanikiwa kutetea taji la Ngao ya Jamii baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba SC kwenye fainali iliyochezwa dakika 90 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa dakika ya 53 na Pacome, ambaye aliwanyanyua mashabiki wa Yanga baada ya kumtungua kipa namba moja wa Simba, Moussa Camara, kufuatia kipindi cha kwanza kilichoisha kwa sare tasa.

Mapema alfajiri ya Septemba 17, 2025, kikosi cha Yanga kilipanda ndege kuelekea Luanda, Angola, kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Ijumaa, Septemba 19, katika Uwanja wa Estádio 11 de Novembro.

Katika msafara huo, miongoni mwa wachezaji waliotajwa ni Dickson Job, Israel Mwenda, Pacome, Djigui Diarra pamoja na Aziz Andambwile.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here