Home KITAIFA KAMWE AMJIBU FADLU NA KUSEMA SISI TUNAO WA MARA TATU

KAMWE AMJIBU FADLU NA KUSEMA SISI TUNAO WA MARA TATU

426
0

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

KAULI ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids kwamba kikosi chake kinakosa mchezaji mwenye uwezo wa kipekee wa kuamua matokeo ya mechi (maarufu kama X-Factor) imeibua majibu kutoka kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.

Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, hakusita kumjibu Davids kwa tambo akibainisha kuwa ndani ya kikosi cha Wananchi kuna wachezaji kadhaa wenye uwezo huo na zaidi.

“Hakuna changamoto ya X-Factor ndani ya Yanga. Tuna wachezaji wengi ambao wanaweza kuibadilisha mechi kwa dakika chache tu. Hata baadhi yao tumeongeza kiwango chao cha ubora kiasi kwamba sasa wana X-Factor tatu,” alisema Kamwe.

Akitaja baadhi ya nyota hao, Kamwe alimtaja Maxi Nzengeli, Clement Mzize na nyota mpya Pacome Zouzoua, akisisitiza kuwa wote ni wachezaji wenye uwezo wa kubeba mchezo mmoja kwa kipaji chao binafsi.

“Huyu Pacome hata msimu uliopita alithibitisha ubora wake. Lakini kuanzia msimu ujao, kutokana na kiwango chake, atakuwa na X-Factor tatu,” aliongeza Kamwe kwa majigambo.

Kauli hii inaendeleza mvutano wa maneno kati ya vigogo hao wa soka la Tanzania, jambo linaloongeza ladha ya ushindani kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here