Klabu ya Barcelona inataka huduma ya nahodha wa Uingereza Harry Kane, 32, ambaye ameifungia Bayern Munich mara 95 katika mechi 102 za ligi. Kane anaonekana kama mbadala wa mshambuliaji Robert Lewandowski.
Vyanzo vya habari nchini Uhispania vinadokeza kuwa Bayern wanaweza kuwa tayari kumuuza Kane kwa kitita cha Euro milioni 40 mpaka 50.
Ikumbukwe mkataba wa Kane na Bayern utatamatika 2027, lakini thamani yake pia itaweza kushuka wakati huo kutokana na umri wake.























