Home KITAIFA YANGA SC YAANZA KUISOMA SIMBA SC KUELEKEA KARIAKOO DABI

YANGA SC YAANZA KUISOMA SIMBA SC KUELEKEA KARIAKOO DABI

302
0
Yanga SC

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC wameanza kupiga hesabu kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC.

Mchezo huo unasubiriwa kwa shauku kubwa unatarajiwa kuwa na ushindani ndani ya dakika 90 kwa wababe hao katika uwanja kusaka ushindi.

Inaelezwa kuwa tayari Kocha Mkuu wa Yanga SC, raia wa Ufaransa, Romain Folz amekabidhiwa video za michezo ya mwisho ya Ligi Kuu Bara ya wapinzani wao Simba SC ambao kwa sasa wapo nchini Misri kwa kambi kuelekea msimu mpya.

Advertisement

Kwa mujibu wa chanzo kutoka ndani ya Yanga SC, video zaidi ya mbili tayari amepatiwa kocha huyo haraka tayari ameanza kuzipitia pamoja na benchi lake jipya la ufundi kuelekea msimu mpya.

Chanzo hicho kilisema kuwa lengo la kupitia video hizo ni kwa ajili ya kuziona mbinu za Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids na wachezaji hatari wa kuchungwa kabla ya kukutana nao Ngao ya Jamii Septemba 16 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here