Home KITAIFA JONATHAN SOWAH KUIKOSA KARIAKOO DABI, UKWELI WOTE HUU HAPA

JONATHAN SOWAH KUIKOSA KARIAKOO DABI, UKWELI WOTE HUU HAPA

231
0
Sowah

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC raia wa Ghana, Jonathan Sowah anatarajiwa kuukosa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC utakaopigwa Septemba 16 2025, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii ni maalumu kwa ajili ya kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Mshambuliaji huyo mpya Sowah hatocheza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye fainali dhidi ya Yanga SC.

Advertisement

Sowah alipata kadi hiyo nyekundu katika mchezo wa Fainali ya Kombe la CRDB ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar akiwa anaichezea Singida Black Stars kabla ya kutambulishwa Simba SC kuwa ingizo jipya na yupo na timu kambini Misri.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo mshambuliaji mpya wa Simba SC, Neo Maema ambaye alitambulishwa Simba SC Agosti 21 2025 akitokea Mamelod Sundowns huenda akabeba mikoba yake kwenye mchezo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here