Klabu ya Manchester United imeripotiwa kumtazama kiungo wa Real Madrid Eduardo Camavinga kuwa mbadala kama watamkosa Carlos Baleba wa Brighton wanayemtazama zaidi kama chaguo la kwanza.
Camavinga aliyekosa nafasi ya kuanza Madrid anatazamiwa kwenda kushindania nafasi na Casemiro, Manuel Ugarte na kinda Kobee Mainoo.