Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home Β» Rasmi Clatous Chama Atibitisha Kurejea Simba
    KITAIFA

    Rasmi Clatous Chama Atibitisha Kurejea Simba

    ChikaoBy ChikaoJanuary 2, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    chama kurejea simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    TETESI za kiungo wa Singida Black Stars, Clatous Chama, kurejea tena ndani ya kikosi cha Simba SC zimezidi kupamba moto, baada ya mchezaji huyo kutoa kauli fupi iliyozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi.

    Chama aliibua hisia hizo kupitia majibu yake kwa shabiki mmoja aliyemkaribisha kurejea Simba, ambapo mchezaji huyo alijibu kwa maneno mawili tu, β€œMapema tu”, kauli ambayo wengi wameitafsiri kama ishara ya wazi ya uwezekano wa kurejea kwake Msimbazi.

    Katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili, jina la Chama limekuwa likihusishwa kwa nguvu na Simba, huku ikielezwa kuwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanatafuta kuimarisha safu ya kiungo kuelekea nusu ya pili ya msimu.

    Mashabiki wa Simba wamekuwa mstari wa mbele kuonyesha mapenzi yao kwa mchezaji huyo kupitia mitandao ya kijamii, wakimiminika na jumbe za kumkaribisha nyumbani pamoja na kumuonesha imani kubwa waliyonayo juu ya uwezo wake.

    Ujumbe mmoja uliovuta hisia za wengi ni ule wa shabiki aliyemwandikia Chama, β€œKaribu Msimbazi mwamba”, ambapo majibu ya haraka kutoka kwa mchezaji huyo yalitosha kuzua mjadala mpana miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka.

    Kauli hiyo imeongeza matumaini kwa mashabiki wa Simba, ambao wanaamini kurejea kwa Chama kunaweza kuipa timu nguvu mpya, hasa katika mbio za mataji ya ndani na mashindano ya kimataifa.

    Ikumbukwe kuwa Clatous Chama aliwahi kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Simba SC katika misimu iliyopita, kabla ya kujiunga na Yanga SC, kisha kuhamia Singida Black Stars msimu huu, huku sasa jina lake likitajwa tena kwa nguvu kuhusishwa na kurejea Msimbazi.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMchezaji Mkongwe Japan asaini mkataba mpya Japan.
    Next Article Msiichukulie Poa Simba ya Sasa, Mazito Yatajwa

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.