Aliyekuwa mtathimini viwango ‘Performance Analysist’ wa klabu ya Simba raia wa Zambia Culvin Mavunga ametangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya misimu mitano aliyodumu ndani ya timu hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa instagram amewashukuru mashabiki na viongozi wa klabu hiyo kwa kipindi chote walichofanya kazi pamoja.
“Ukurasa wangu na Simba SC imefika mwisho. Imekuwa misimu 5 ya kuvutia na timu. Tulishinda, tukashindwa na kutoka sare pamoja.
“Pongezi zangu za dhati ziwaendee Mashabiki wa Simba, nyie watu wa muhimu, kwa Bodi na Uongozi wa Simba, asante kwa kila jambo. Kwa Benchi la Ufundi la Simba, upendo sana na nyinyi ni familia daima. Kwa Wachezaji wa Simba nawapenda sana familia. Kwa Kocha Fadlu, asante kwa mafunzo🙏🏾”
“Nawatakia wote msimu wenye Mafanikio.Kurasa MPYA na Mwanzo Mpya unanisubiri.Endelea kubarikiwa 🙏🏾”Ameandika Mavunga.