Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars imejiondoa kwenye mashindano ya CECAFA yanayojumuisha timu nne, yaani Tanzania, Kenya, Uganda na Senegal ikiwa ni masaa machache kabla ya kutakiwa kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Uganda majira ya saa 9 jioni.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la mpira la Nchi hiyo limeweka wazi kuwa sababu ya timu hiyo kujiondoa ni baada ya kocha mkuu wa Taifa hilo Benni McCrthy kutoridhishwa na mazingira ya mashindano hayo.
Awali timu ya taifa ya CONGO BRAZA VILLE ilijiondoa kwenye mashindano hayo wiki moja kabla ya michuano hiyo kuanza kutokana na kupata changamoto ya kusafiri, na baadaye Senegal ikajitokeza kuziba pengo la timu hiyo.
Licha ya kuwa timu hiyo tayari ilikuwa imefika Jijini Arusha na kufanya mazoezi ya mwisho siku ya jana imelazimika kuanza safari ya kurejea nchini kwao Kenya kuendelea na maandalizi ya CHAN ambayo itaanza tarehe 02/08/2025.