INAELEZWA kuwa nyota wa zamani wa Yanga SC, Clatous Chama anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Singida, Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti.
Chama aliwahi kucheza Simba SC kabla ya kuibukia ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25 akiwa mchezaji huru na hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na uwepo wa Aziz KI.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga SC hawana mpango na Chama mara baada ya mkataba wake kuisha hivyo atasajiliwa na Singida Black Stars akiwa mchezaji huru.
Chama alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC na Zesco United ambapo huko alikuwa anafanya mazoezi licha ya kwamba hajasaini.
Singida Black Stars kwa sasa inanolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye aliwahi kufanya kazi na Chama katika kikosi cha Yanga SC.