KITAIFA

HUYU HAPA KAPEWA MAJUKUMU YA USAJILI SIMBA SC, ASEMA MTULIE

fadlu simba

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC msimu wa 2025/26 wameweka wazi kuwa mpango kazi wa kufanya usajili upo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Simba SC iligotea nafasi ya tatu kwenye msimamo ikapeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa msimu wa 2024/25 iligotea kuwa mshindi wa pili Kombe la Shirikisho Afrika na bingwa alikuwa ni RS Berkane.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu ujao ni kufanya vizuri zaidi na watafanya usajili makini.

“Kwenye kufeli msimu uliopita ni sehemu ya matokeo kwa kuwa bado tunajenga timu hilo lieleweke na mashabiki wasikate tamaa wala wasiishiwe pawa. Kikubwa ni mshikamano na kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano.

“Kwa msimu huu asilimia kubwa suala la usajili litakuwa mikononi mwa Kocha Mkuu, Fadlu Davids, yeye atasimamia kila kitu na viongozi watakamilisha mpango kazi.”

Leave a Comment