Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » KIBU NAYE KUIPA ‘THANK YOU’ SIMBA?….WAMAREKANI WAZIDI KUDATA NAYE KILA SIKU
    KITAIFA

    KIBU NAYE KUIPA ‘THANK YOU’ SIMBA?….WAMAREKANI WAZIDI KUDATA NAYE KILA SIKU

    ChikaoBy ChikaoJuly 22, 202502 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    kibu
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    NDOTO ya mshambuliaji wa Simba SC na Taifa Stars, Kibu Dennis kucheza soka la kulipwa Marekani inakaribia kutimia baada ya klabu ya Nashville kumwongezea wiki ya majaribio kutokana na kile kinachoelezwa ni kivutio kwa makocha wa kikosi hicho.

    Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya karibu na mchezaji huyo, Kibu ambaye yuko Marekani tangu mwisho wa mwezi Juni, alikuwa amepewa wiki mbili za awali za kuonyesha uwezo wake.

    Hata hivyo, baada ya kipindi hicho kukamilika, uongozi wa Nashville SC inayoshiriki Ligi Kuu Marekani umevutiwa na mwenendo wake na kuamua kumwongeza wiki nyingine ya tathmini ya kiufundi.

    “Kibu anapambana kweli kweli,” alisema mmoja wa watu wa karibu na nyota huyo aliyeko jijini Nashville.

    “Hapa soka siyo lelemama. Wachezaji wapo wengi, ushindani ni mkubwa. Lakini mpaka kumpa wiki ya tatu, ina maana ana kitu cha ziada.”

    Klabu hiyo inayoshika nafasi ya pili kwenye kundi la Mashariki katika Ligi Kuu ya Marekani, imekuwa na mpango wa kuimarisha kikosi chake hasa upande wa winga mwenye kasi na uwezo wa kucheza namba 7 na 11, ambayo Kibu anaweza kucheza kwa ufanisi mkubwa.

    Chanzo cha kuaminika kutoka Marekani, kilinukuliwa na gazeti la  Mwanaspoti: “Majaribio yanafanyika na kikosi cha pili (reserve team), lakini waamuzi ni benchi kuu la ufundi. Walianza na wachezaji watano, baada ya wiki mbili watatu walikatwa. Kibu na kijana mmoja kutoka Brazil ndio waliobaki na kuongezewa muda kwa sababu walionesha kitu.”

    Kwa upande mwingine, taarifa kutoka Simba SC zinaeleza, iwapo Kibu atafaulu majaribio hayo, Nashville SC italazimika kuwasilisha ofa rasmi ya kumnunua mchezaji huyo, ambaye bado ana mkataba na Wekundu wa Msimbazi hadi mwishoni mwa msimu ujao.

    Katika mazungumzo ya awali, kocha wa kikosi cha pili cha Nashville, Michael Nsien ambaye ni msaidizi wa kikosi cha kwanza alieleza kuvutiwa na ubora wa Kibu katika kupiga pasi, kasi, pamoja na uwezo wa kumiliki mpira katika presha.

    Hiyo ndiyo sababu inayoelezwa kumtazama kwa karibu zaidi.

    Mdau wa soka wa Tanzania anayeishi mjini Nashville, Abdallah Karim, amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti:

    “Waafrika wako wachache kwenye kikosi hiki. Kibu ana nafasi nzuri sana. Kama akijituma wiki hii, naamini anaweza kumsajili, hii timu ina uwezo mkubwa kifedha.”

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleHUYU HAPA KAPEWA MAJUKUMU YA USAJILI SIMBA SC, ASEMA MTULIE
    Next Article KOCHA WA MAMELOD SUNDOWN KUULA YANGA….JAMAA ANA MIAKA 34 TU

    Related Posts

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    March 24, 2026

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    March 24, 2026

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    March 24, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HII HAPA SABABU KUBWA YA MPANZU KUTO WASALITI SIMBA

    UAMUZI WA KIUFUNDI WAMUWEKA MPANZU SIMBA

    DIARRA AWEKA REKODI, AMUACHA MBALI KIPA WA SIMBA

    Yanga Yamrudisha Kocha Abdihamid Moalin Kuinua Kiwango cha Timu

    Zidane Kurithi Mikoba ya Deschamps Ufaransa Baada ya Kombe la Dunia 2026

    Katibu wa Senegal asema Kombe halitaondoka Nchini kwao.

    FIFA YAPITISHA SHERIA MPYA 6 KUELEKEA KOMBE LA DUNIA 2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.