YANGA SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika wakiwa na mataji 31 kabatini wametambulisha nyota watatu ndani ya Agosti 2025. Katika wachezaji hao usajili ambao ulitikisa ni ule wa beki Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyetambulishwa hapo akitokea kikosi cha Simba SC baad
MECHI ya Simba na Yanga inatarajiwa kuchezwa mapema ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayowakutanisha Yanga SC na Simba SC, Septemba 16, 2025 jijini Dar. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa kwa mwaka huu, Ngao
MASTAA wa kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu,Romain Folz Agosti 19 2025 walikuwa kwenye mazoezi maalumu katika fukwe za Coco Beach Dar kwa lengo la kusaka pumzi na kuwa imara zaidi. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Af
MSHAMBULIAJI namba moja kwa wazawa wenye mabao mengi msimu wa 2024/25 Clement Mzize bado ana mkataba na Yanga SC kuelekea msimu wa 2025/26. Mzize amekuwa akitajwa kuwa katika rada za timu mbalimbali ambapo kuna timu moja kutoka Tunisia inatajwa kuweka dau kubwa mezani kupata saini yake kwa ajili ya
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe ameweka wazi kuwa kuna ugumu wa kufanya sherehe za wiki ya wananchi kwa mwaka huu kutokana na ugumu wa ratiba na upatikanaji wa uwanja. “Tunapamba siku ya Wananchi iwepo lakini kuna changamoto nyingi tunapitia, ukiangalia mashindano ya CHAN y
Ifahamu Gaborone United Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa CAF 2025/2026 Wababe wa kulisakata kabumbu wa Tanzania Bara na Visiwani Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Singida Black Stars, KMKM na Mlandege SC wameshajua wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kwa hat
….. OFA IMEKATALIWA. Jana tulilala na neno hili. Barua za Waarabu zimeendelea kupishana pale Jangwani. Inaingia barua hii, baada ya muda inaingia barua nyingine. Zote zinazungumzia upatikanaji wa Mzize. Wanachokifanya Yanga SC ni kumtafuta yule mwenye kisu kikali ndio ale nyama. Mimi siamini kama Mz
Mabingwa wa soka la Tanzania, Yanga SC wamepangiwa timu ya Wiliete Benguela ya nchini Angola. Ratiba hiyo ya CAF imetoka leo na Yanga SC wameangukia kwa vigogo hao wa soka la nchini Angola.
KAMA unadhani Yanga SC mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamemaliza usajili, bado kazi haijaisha kwa kuwa kuna wachezaji wengine wapya bado hawajatambulisha. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa mara 31 wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC hii ni ligi namba nne kwa ubora Afrika.Ni point
YANGA SC mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26 hawapoi kutokana na kasi yao kwenye utambulisho wa wachezaji wapya. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Yanga SC ilitwaa taji la Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC likiwa ni taji lao la 31. Baada ya mechi 30 walikusanya jumla ya po
Kuelekea msimu wa 2025/26, Uongozi wa Young Africans leo asubuhi umekutana na Benchi la ufundi, wachezaji na watendaji wa Klabu kwa ajili ya utambulisho na semina kuhusu historia, matarajio na majukumu ya kila mmoja ndani ya Klabu Hafla hii imefanyika kwenye hoteli ya Rotana, Jijini Dar Es Salaaam.
Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli (24) kama mchezaji mpya wa kikosi hicho kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja kutoka Sekhukhune United ya Afrika Kusini, ukiwa na kipengele cha kununuliwa kabisa mwishoni mwa mkataba. Boyeli anasifika kwa uwezo mkubwa wa kufumania nyav
INAELEZWA kuwa nyota wa zamani wa Yanga SC, Clatous Chama anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Singida, Singida Black Stars inayotumia Uwanja wa Liti. Chama aliwahi kucheza Simba SC kabla ya kuibukia ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25 akiwa mchezaji huru na hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutok
Kiungo mahiri kutoka Ivory Coast, Pacome Zouzoua,inasemekana ameshasaini mkataba mpya na klabu ya Yanga SC siku nyingi zilizopita, muda mfupi tu baada ya fainali ya Kombe la CRDB. Kwa mujibu wa taarifa za ndani, mkataba huo wa miaka miwili ulitayarishwa na kusainiwa kipindi hicho, huku mpunga ukisha
Katika kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili, habari kuhusu wachezaji wakuu na usajili wao huwa kivutio cha umma. Miongoni mwao ni Ellie Mpanzu, kiungo mahiri wa Simba SC, ambaye hivi karibuni amezungumzia uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.