Home KITAIFA SIMBA KUMSHUSHA BEKI WA MAMELODI SUNDOWNS RUSHINE DE REUCK

SIMBA KUMSHUSHA BEKI WA MAMELODI SUNDOWNS RUSHINE DE REUCK

58
0
simba

Klabu ya Simba inatajwa kumalizana na beki wa kati wa klabu ya Mamelodi Sundowns aliyekuwa anakipiga kwa mkopo Maccabi Petah Tikva ya ligi kuu ya Israel Rushine De Reuck mwenye umri wa miaka 29.

Tetesi zinasema nyota huyo anajiunga na wekundu wa msimbazi Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja baada ya mkopo wake ndani ya Maccabi kutamatika.

Nyota huyo aliyecheza mechi 4 pekee katika ligi kuu ya Israel kutokana na machafuko yaliyokuwa yanaendelea Nchini humo taarifa zinasema kuwa na chaguo la kocha Fadlu kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi.

Rushine ambaye ni raia wa Afrika Kusini ameshawahi kutwaa tuzo ya beki bora wa ligi kuu ya Afrika Kusini kabla ya kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundowns.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here