Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amethibitisha tetesi zilizoshika kasi siku ya jana kuhusu mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah kutua unyamani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ahmed Ally amechapisha picha ya DJ maarufu anayefanya kazi na klabu yake DJ Sinyorita huku akiambatanisha na ujumbe ufuatao;
“DJ Sinyorita tuwekee wimbo wa sitaki mazoea tumtambulishe Sowah halafu hapo kwenye sitaki mazoea rudia rudia”Ameandika Ahmed Ally.