NI wazi kuwa Tanzania imeng’ara baada ya mwakilishi pekee kinda Mtanzania, Harrith Chunga Misonge mwenye umri wa miaka 12 kuwa gumzo.
Misonge mkazi anaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Phygital Football for Friendship akiwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Mwakilishi mwingine ni mtoto kutoka Afrika ya Kati lakini hajang’ara kama Misonge ambaye amepewa nafasi ya uongozi katika kiongozi.
Viongozi wa watoto hao wamemsifia kwa uwezo wa kucheza soka lakini pia ni kiongozi na wakati wa ufunguzi yeye aliwaongoza wenzake.
Ni mtoto mtaratibu mwenye kipaji na leo ni Mtanzania mwakilishi wa Afrika barani Ulaya kwenye michuano mikubwa ya watoto kujenga umoja, undugu na urafiki lakini kujifunza mambo mengi yakiwemo ya maisha.
Russia imeona kuna nafasi ya kuwasaidia watoto kuungana na kuiunganisha dunia kutumia watoto.
Harrith, mwanafunzi katika shule ya Aghakhan anakuwa sehemu ya mwanga kwa watoto wa Kitanzania kuwa INAWEZEKANA.
Mwaka jana alifanya vema katika michuano ya Gothia nchini Sweden na sasa nyota yake inag’ara hapa katika jiji la Kazan.