YANGA YASHINDA TUZO YA TIMU BORA YA KIUME, WASHINDI WAPO HAPA WA TUZO ZA BMT 2023
Klabu ya Yanga imefanikiwa usiku wa kuamkia leo Juni 10, 2024 kushinda tuzo ya Timu bora ya Kiume ya Mwaka 2023 kwa ngazi ya vilabu kwenye tuzo zinazotolewa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
Ndani ya mwaka huo Yanga ilitwaa Ubingwa Ligi kuu, Ubingwa FA, Ngao ya Jamii sambamba na kufanikiwa kufika fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.
Pia Timu ya taifa ya wanaume ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshinda tuzo ya Timu bora ya kiume Mwaka 2023 kwa ngazi ya taifa kwenye tuzo zinazotolewa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT)
Washindi wengine wa tuzo hizo za BMT 2023
Tuzo ya Mwandishi bora wa Michezo wa kiume imeenda kwa Hussein Shafih kutoka Shirika la Utangazaji TBC
Mwandishi bora wa Michezo wa kike ni Fatma Chikawe kutoka Azam Media
Ahmed Arajiga Mwamuzi bora wa kiume wa Mwaka tuzo za BMT
Mwamuzi bora wa kike wa Mwaka ni Pendo Njau
Tuzo ya mwanamichezo bora chipukizi wa kiume imekwenda kwa Romeo ambaye ni mkali wa kuogolea.
Mwanamichezo bora wa kiume mwaka 2023 ni bondia Yusuph Changalawe.
Tuzo ya Timu Bora ya klabu kwa upande wa wanawake, imekwenda kwa JKT Queens.
Mwanamichezo bora wa kike mwaka 2023 ni bondia bondia Grace Mwakamele.
Timu ya Taifa ya Wanawake upande wa kriketi imetwaa Tuzo ya Timu Bora ya Taifa upande wa Wanawake.
Bondia Grace Mwakamele ndiye Mwanamichezo Bora wa kike mwaka 2023
Vosta Isaya Lengonela wakati akipokea tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa wenye ulemavu.
Tuzo ya heshima kwa nahodha wa zamani wa Taifa Stars ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
Mwanamichezo bora wa kike kutoka shuleni ni Happiness Fabian Kongoka kutoka Kapuya Sekondari, Kaliua Tabora.
Tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume kutoka shuleni imekwenda kwa Agape Mwenda