Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema mazungumzo ya kandarasi za Bukayo Saka na William Saliba yanakwenda vizuri.
Wachezaji hao wawili muhimu wa Arsenal mikataba yao inategemewa kutamatika 2027, na sasa Washika Bunduki hao wa jiji la London wapo kwenye majadiliano mazito na wachezaji hao ili waweze kuwaongezea mikataba.
“Nadhani jambo zuri ni kwamba wachezaji wanataka kubaki hapa na wanataka kuwa sehemu kubwa ya historia ya klabu hii katika miaka michache ijayo na hilo ni jambo jema.” alisema Arteta