Home KITAIFA KIUNGO MPYA YANGA SC AJIPA KAZI, YANGA DAY INANUKIA

KIUNGO MPYA YANGA SC AJIPA KAZI, YANGA DAY INANUKIA

1109
0
yanga

YAKIWA yamebaki masaa kabla ya tukio la Yanga Day kufanyika, kiungo mpya katika timu hiyo amejipa kazi nyingine ngumu ili awe imara zaidi.

Ikumbukwe kwamba kesho Septemba 12, Yanga SC itakuwa na tukio la utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi msimu wa 2024/25.

Offen Chikola ambaye huyu ni ingizo jipya akitokea Tabora United ameomba ruhusa kwa kocha wake Mfaransa, Romain Folz ya kutoka kambini na kwenda gmy kufanya mazoezi binafsi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Yanga, kiungo huyo ameomba ruhusa ya kufanya mazoezi muda wa mapumziko kwa ajili ya kujiweka sawa kuelekea msimu mpya wa 2025/26/

Haya yote yanafanyika ili kuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ya NBC ambayo inatarajiwa kuanza Septemba 17 2025.

Yanga SC kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi wanatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Bandari, Uwanja wa Mkapa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here