KITAIFA

SIMBA SC YASAKA KIPA KUMPA CHANGAMOTO CAMARA

simba

SIMBA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini ipo katika harakati za kumsajili kipa wa JKT Tanzania, Yakoub Seleman katika msimu ujao.

Kipa namba moja kwa sasa ndani ya Simba SC ni Moussa Camara. Ni hati safi 19 amekusanya msimu wa 2024/25 akiwa kipa namba moja mwenye hati nyingi ndani ya ligi namba nne kwa ubora.

Inaelezwa Simba SC wanamtaka kipa huyo haraka na hivi sasa wapo katika harakati za mwishoni za kimyakimya za kumpata Yacoub.

Simba SC kama watampata kipa huyo, basi wataachana na Hussein Abel katika msimu ujao ambaye ni kipa namba tatu wa timu hiyo iliyogotea nafasi ya pili msimu wa 2024/25.

Ipo wazi kwamba mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni Yanga SC ambao kipa wao namba moja ni Djigui Diarra chaguo la kwanza la Miloud Hamdi.

Leave a Comment