KITAIFA

YANGA YATANGAZA KULITAKA KOMBE LA CRDB

yanga

UONGOZI wa Klabu ya Yanga SC umeweka wazi dhamira yao ya kuhakikisha wanarejesha nyumbani Kombe la CRDB Federation Cup, wakisisitiza kuwa wao ni mabingwa watetezi licha ya kupangwa kucheza dhidi ya timu ngumu, Singida Black Stars, kwenye fainali.

Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuchezwa leo, Jumapili, Juni 29, 2025, ambapo macho ya Watanzania wengi yataelekezwa kwenye uwanja huo mkubwa wa kihistoria.

Yanga SC inashuka dimbani ikiwa na morali ya juu, baada ya kutwaa taji la 31 la Ligi Kuu Bara, kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya watani wa jadi Simba SC. Klabu hiyo imemaliza ligi ikiwa na pointi 82, ikifunga mabao 83 na kuruhusu mabao 10 tu – rekodi ya juu kwa msimu huu.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema:

“Singida Black Stars walitusumbua kweli kwenye mechi zetu mbili za ligi. Kuelekea mchezo wetu wa fainali, tupo tayari na tunalitaka kombe letu, licha ya ugumu ambao upo mbele yetu. Tunaamini benchi la ufundi na wachezaji watakamilisha majukumu yao.”

Leave a Comment