Home KITAIFA TAIFA STARS KUINGIA KAZINI LEO

TAIFA STARS KUINGIA KAZINI LEO

113
0
stars

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Septemba 5 2025 kitakuwa kazini kwenye mchezo dhidi ya Congo Brazzaville ambao ni maalumu kwa ajili ya kufuzu kombe la Dunia 2026 utakaochezwa  Uwanja wa Alphonce Masamba Debat.

Septemba 4 2025 Stars ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa ambao utatumika kwa mchezo wa leo kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleman.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo katika kikosi cha Stars ni Simon Msuva, Mbwana Sammatta, Dickson Job, Clement Mzize, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, Nado, Bacca.

Ikumbukwe kwamba Stars imetoka kushiriki CHAN 2024 ikigotea hatua ya robo fainali na mabingwa walikuwa ni Morocco ambao waliwafungashia virago Stars kwenye hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mkapa.

Septemba 9 2025 Taifa Stars itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Niger ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here