Home KIMATAIFA NEYMAR AACHIWA URITHI WA TRIL 2+ NA MTU ASIEMJUA

NEYMAR AACHIWA URITHI WA TRIL 2+ NA MTU ASIEMJUA

243
0

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

Nchini Brazil kumeibuka simulizi ya kushtua baada ya bilionea mwenye umri wa miaka 31 kutoka jimbo la Rio Grande do Sul kuamua kumwachia nyota wa soka Neymar Jr mali zake zote, licha ya wawili hao kutokuwa na uhusiano wowote wa karibu au hata kukutana ana kwa ana.

Kwa taarifa za vyombo vya habari vya kimataifa, kijana huyo tajiri hakuwa na mke wala watoto, na mwezi Juni 2025 aliandika wosia rasmi katika ofisi ya serikali ukiwa na mashahidi. Katika hati hiyo alielekeza majumba, kampuni na vitega uchumi vyake vyote vyenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1 (takribani shilingi trilioni 2.5 za Kitanzania) viende kwa Neymar pekee.

Sababu ya uamuzi huo imetajwa kuwa ni heshima na imani yake kwa utu wa Neymar, hususan unyenyekevu na ukaribu wake na baba yake, kitu kilichomvutia sana bilionea huyo.

Kwa sasa, urithi huo mkubwa unasubiri kupitishwa kisheria na mahakama za Brazil kabla ya kuhamishiwa rasmi kwa staa huyo wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Brazil.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here