Home KITAIFA HII HAPA RATIBA YA NBC PREMIER LEAGUE

HII HAPA RATIBA YA NBC PREMIER LEAGUE

31
0

NBC Premier League tayari pazia lake limefunguliwa na Septemba 17 mechi mbili za ufunguzi zilichezwa.

KMC 1-0 Dodoma Jiji huu ulichezwa Uwanja wa KMC Complex na mtupiaji wa bao la kwanza msimu wa 2025/26 ni Daruesh Saliboko dakika ya 56 likidumu mpaka mwisho wa dakika 90.

Mchezo wa pili ilikuwa Coastal Union 1-0 Tanzania Prisons huu ulichezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bao la Coastal Union lilifungwa na Cleofance Mkandala dakika ya 35.

Septemba 18 2025 kuna mechi tatu ambazo zinatarajiwa kuchezwa itakuwa namna hii:-

Saa 8:00 mchana, Fountain Gate watakuwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa vs Mbeya City.

Saa 10:15 jioni Mashujaa vs JKT Tanzania, Uwanja wa Lake Tanganyika.

Saa 1:00 usiku, Namungo FC vs Pamba Jiji, Uwanja wa Majaliwa.

Septemba 20 2025 kutakuwa na mchezo mmoja Tabora United vs Dodoma Jiji utachezwa saa 8:00 mchana.

Septemba 21 2025 kutakuwa na mechi mbili, Mashujaa FC vs Mtibwa Sugar saa 10:00 jioni na Namungo FC vs Tanzania Prisons itakuwa saa 1:00 usiku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here