Home KIMATAIFA HAZARD ANAAMINI MESSI NDIO MPIGA CHENGA ZAIDI KULIKO YEYE

HAZARD ANAAMINI MESSI NDIO MPIGA CHENGA ZAIDI KULIKO YEYE

76
0

JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA

Nyota wa zamani wa Chelsea na Real Madrid, Eden Hazard ametupilia mbali mastaa Cristiano Ronaldo, Lamine na Neymar huku akimtaja Lionel Messi kuwa ndiye mpiga chenga mkali kuliko yeye.

Hazard alizungumza hayo katika video iliyorushwa kwenye akaunti ya X ya UEFA Champions League.

Kwenye video hiyo mwanasoka huyo mstaafu aliombwa kutulia (kukaa kimya) hadi atakaposikia jina la mwanasoka, ambaye anaamini alikuwa mpiga chenga bora kuliko yeye.

Katika orodha hiyo majina yalianza kama ifuatavyo; Desire Doue wa Paris Saint-Germain, Rafel Leao wa AC Milan, Khvicha Kvaratskhelia wa Paris Saint-Germain, na Raphinha wa Barcelona, lakini Hazard alikaa kimya.

Uso wake ukashtuka kidogo baada ya kutajwa jina la Riyad Mahrez winga wa zamani wa Manchester City na jina la winga wa Real Madrid Vinicius Jr, lakini alikaa kimya.

Hata baada ya kutajwa majina ya Christiano Ronaldo na Lamine Yamal aliendelea kukaa kimya.

Lilipotajwa jina la Neymar alitafakari kidogo na kuendelea kukausha, hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alivunja ukimya lilipotajwa jina la Messi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here