JIUNGE KWENYE WHATSAPP CHANNEL YA SIMULIZI ZA SAUTI ZA WAKUBWA TU BONYEZA HAPA KUJIUNGA
Mgombea Udiwani Kata ya Kariakoo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Haji Manara, amekutuna na kufanya kikao na Mtumishi wa Mungu kutoka Kanisa la Arise and Shine International, Mtume Boniface Mwamposa leo, Septemba 3, 2025.
Kikao hicho kimefanyika Jijini Dar es Salaam na kimekuwa na lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya viongozi wa kisiasa na wa kidini, hasa katika masuala yahusuyo maendeleo ya Jamii na ustawi wa wananchi wa Kariakoo na Tanzania.
Wiki iliyopita Manara alikutana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Bin Zubeir na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa nchini, Sheikh Hassan Chizenga ambao walimuombea Dua.
Manara amemshukuru Mtume Mwamposa kwa mapokezi na kwa kuonesha utayari wa kushirikiana katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.
Mtume Mwamposa amepongeza juhudi za mgombea huyo na kuahidi kuendelea kushirikiana naye katika kuhakikisha ustawi na maendeleo ya wananchi, hasa kwa kuhakikisha jamii inakuwa na maadili na nidhamu.