Mshambuliaji mpya wa Timu ya Taifa Stars Suleman Mwalimu amewasili jijini Dar es salaam kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Athletic.
Mwalimu ambaye alikiwasha ligi kuu Tanzania bara akiwa na Singida BS na Fountain Gate atasalia jijini Dar es akiendelea na mazoezini binafsi mpaka pale kikosi cha Simba kitakaporejea nchini kutoka Misri kilipoweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya.
Simba itarejea Alhamisi ya Agosti 28 baada ya kukamilisha wiki nne za mazoezi katika kambi waliyokuwa wameiweka Ismailia na Cairo Nchini Misri.