Home KIMATAIFA ROONEY AWAONYA LIVERPOOL JUU YA MCHEZAJI ‘ISACK’ KUIGOMEA NEWCASTLE

ROONEY AWAONYA LIVERPOOL JUU YA MCHEZAJI ‘ISACK’ KUIGOMEA NEWCASTLE

85
0
Rooney

Wayne Rooney ameonya kuwa Liverpool wanapaswa kuwa makini kabla ya kukamilisha usajili wa Alexander Isak, huku mshambuliaji huyo wa Sweden akikataa kuchezea Newcastle United.

Isak, mwenye umri wa miaka 25, amedhamiria kuondoka Newcastle katika dirisha hili la usajili baada ya kufunga mabao 23 kwenye Ligi Kuu ya England msimu uliopita. Hata hivyo, hatua yake ya kuripoti jeraha ili asijihusishe na mazoezi ya timu imeibua mjadala mkubwa.

Mshambuliaji huyo alisafiri hadi Uhispania kufanya mazoezi binafsi katika uwanja wa zamani wa Real Sociedad, wakati Liverpool wakitarajiwa kuwasilisha ofa ya pili katika wiki zijazo.

Advertisement

Kwa sasa, Isak amegoma kuchezea kikosi cha Eddie Howe, hatua iliyopingwa na Rooney pamoja na mchambuzi mwenzake Alan Shearer wakati wa kipindi cha Match of the Day Jumamosi usiku.

Akizungumza na mtangazaji Mark Chapman, Rooney alisema:

“Kama ni kweli anakataa kufanya mazoezi na wenzake, itakuwa vigumu sana kwake kurejea. Kuna suala la uaminifu hapa, na anaishughulikia vibaya. Huenda anashauriwa vibaya. Lakini kwa timu inayotaka kumsajili, kwa mfano Liverpool, inabidi ujiulize kama huyu ndiye aina ya mchezaji unayemtaka – ambaye anawaacha wachezaji wenzake na klabu yake.”

Rooney aliongeza kuwa fursa ya kujiunga na klabu kubwa ni nzuri, lakini ni lazima Isak ashughulikie suala hili kwa nidhamu na njia sahihi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here