Home KITAIFA MZIZE KULIPWA MSHAHARA MREFU YANGA SC

MZIZE KULIPWA MSHAHARA MREFU YANGA SC

57
0
Yanga SC

MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Clement Mzize kuna uwezekano mkubwa akabaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2025/26 na atakuwa anakunja mshahara mrefu kwa mwezi.

Taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa Mzize kuna timu ambazo zinahitaji huduma yake kutoka Ulaya jambo ambalo lilikuwa linasubiriwa ni kuisha kwa mashindano ya CHAN. Wakati mashindano yanaendelea Tanzania imeishia hatua ya robo fainali.

Taarifa zinaeleza kuwa Mzize ambaye kwenye ligi alifunga mabao 14 akiwa mshambuliaji mzawa mwenye mabao mengi katika CHAN a2024 alifunga mabao mawili huenda hataondoka kwa ajili ya changamoto mpya atasalia Yanga SC.

Advertisement

Mshambuliaji huyo inatajwa kuwa alikaa kikao na viongozi wa Yanga SC wakifikia makubaliano ya kuongeza mshahara wake na posho.

Kwa mujibu wa chanzo cha Habari kutoka ndani ya Yanga, mshambuliaji huyo amefanyiwa maboresho ya mshahara wake ambao unafikia zaidi ya milioni 45 atakaoupata hadi msimu 2026/27.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alizungumzia hilo kwa kusema kuwa “Zipo ofa mbili kutoka ndani nan je ya Afrika zikimuhitaji Mzize, Uongozi unazipitia hivi sasa lakini ikumbukwe bado mchezaji wa Yanga hadi 2027.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here