Jicho la kiungo mkabaji wa kikosi cha timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Ahmed Bakari ‘Pipino’ @_ahmed_pipino limevimba baada ya kupigwa kiwiko katika mchezo wa jana wa Stars dhidi ya Mauritania.
Pipino alipata jeraha hilo lililomfanya ashindwe kuendelea na mchezo huo na akatolewa na nafasi yake akaingia kiungo mwingine Shekhan Khamis.
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Shomary Kapombe.