MSHAMBULIAJI mpya wa Simba SC 2025/26 Jonathan Sowah raia wa Ghana ametuma ujumbe kwa mashabiki kwa kubainisha kuwa watafurahi msimu mpya. Nyota huyo yupo kambini nchini Misri chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Sowah alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC akitokea Singida Black Stars. Msimu wa 2024/25 alifunga jumla ya magoli 13. Katika mabao hayo aliwafunga watani wa jadi Yanga SC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
“Mimi Jonathan Sowah ni Simba mweusi. Ninapenda kuwaambia mashabiki wa Simba SC kuwa watafurahi. Kwa kila shabiki ambaye atakuja uwanjani na yule ambaye atakuwa nyumbani hakika atafurahi.
“Kuna mengi ambayo tunaamini tutafanya. Ushirikiano mkubwa kwa wachezaji na benchi la ufundi. Hakika kila mmoja atafurahi, mashabiki tuzidi kuwa pamoja.”