MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC Yanga SC wanatarajiwa kuelekea Rwanda. Timu hiyo inaenda Rwanda kwa mualiko maalum kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki. Mchezo huo unatarajiwa kuwa dhidi ya kikosi cha Rayon Sports.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema: “Hivi karibuni tulizindua kampeni ya Tofali la ubingwa. Hii ililenga kuwapa wanachama nafasi ya kuchangia timu yao kwa ajili ya kuipa misuli ya kifedha.
“Mahitaji haya ni kwa ajili ya kufanikisha usajili na maandalizi ya kambi ya kabla ya msimu ‘Pre-season’. Ikumbukwe maandalizi ni bora ili kuweza kutimiza malengo yetu ya ubingwa kwa msimu mzima. Tayari tumepata mwaliko wa kwenda Rwanda kwa ajili ya kushiriki siku ya kilele cha klabu ya Rayon Sports.
Kwa sasa timu ya Yanga SC inaendelea kusukwa, na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundowns Roman Folz. Kocha huyo ni miongoni mwa wakufunzi wenye wasifu mkubwa na uzoefu na sola la Afrika.
Folz na benchi lake jipya la ushindi tayari wameanza rasmi majukumu yao ya kuinoa Yanga. Hii ni kupitia kambi ya maandalizi kabla ya msimu ‘Pre-season’ inayoendelea kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.