Home KIMATAIFA GREALISH ATAMBULISHWA RASMI EVERTON

GREALISH ATAMBULISHWA RASMI EVERTON

74
0

Everton wametangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Jack Grealish kwa mkopo kutoka Manchester City.

Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 29 ataitumikia The Toffees msimu mzima wa 2025/26 na atavaa jezi namba 18. Grealish, ambaye ameshinda mataji makubwa akiwa na City ikiwemo Ligi Kuu mara tatu, Kombe la FA mara mbili, Ligi ya Mabingwa, UEFA Super Cup na Kombe la Dunia la Klabu, anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na David Moyes majira haya ya joto baada ya kuwasili kwa Charly Alcaraz, Thierno Barry, Mark Travers, Adam Aznou na Kiernan Dewsbury-Hall.

Akihojiwa na Everton Tv, Grealish alisema: “Nimefurahi sana kusaini Everton. Ni jambo kubwa kwangu, kwa kweli. Hii ni klabu kubwa yenye mashabiki wakubwa. Nilipozungumza na kocha, nilijua hakuna sehemu nyingine ningependa kwenda. Mashabiki wamekuwa wakinitumia ujumbe mwingi wa kunikaribisha, na hiyo pia ilinifanya nichague kujiunga na Everton. Asanteni kwa upendo na sapoti, natumai nitawalipa kwa kile nitakachotoa uwanjani.”

Advertisement

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here