Home KITAIFA FEISAL SALUM AFICHUA HESABU ZA TANZANIA CHAN 2024

FEISAL SALUM AFICHUA HESABU ZA TANZANIA CHAN 2024

86
0

WAKATI Tanzania Agosti 16 2025 kwenye mchezo wa CHAN 2024 ikishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Afrika ya Kati 0-0 Tanzania, kiungo Feisal Salum amebainisha kuwa watapambana katika hatua ya robo fainali kupata matokeo mazuri.

Mchezo huo uliopita hatua ya makundi ulikuwa wa kwanza kwa Tanzania kugawaa pointi mojamoja. Katika mechi tatu ambazo zilipita za makundi Tanzania ilishinda zote ikikusanya pointi 9.

Baada ya mechi nne, Tanzania inaongoza kundi B ikiwa na pointi 10 itacheza na Morocco hatua ya robo fainali mchezo unaotarajiwa kuchezwa Agosti 22, 2025 Uwanja wa Mkapa.

Advertisement

Nyota huyo ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya mchezo alibainisha kuwa wanatambua kuna kazi kubwa mbele yao hivyo watapambana kuwa bora zaidi.

“Kwenye mchezo wetu uliopita haikuwa shida katika kutafuta matokeo kwa kuwa tulienda na game plan yetu ya kile ambacho tulifundishwa mazoezini. Ambacho walifanya wapinzani wetu ni kuziba nafasi ambazo tulizifanyia mazoezi. Mimi mchezaji katika matokeo tuliyopata hatujaridhika.

“Tulitegemea matokeo kwenye mchezo wetu. Wenzetu walituheshimu na kuja kwa umakini. Mchezo huu umepita tunaangalia mechi zijazo hatua ya robo fainali. Tunaamini tutapambana kufanya vizuri zaidi, “ amesema Fei Toto

Kocha Mkuu wa Tanzania, Hemed Suleman ameweka wazi kuwa makosa yaliyopita watafanyia kazi ili kupata matokeo kwenye mechi zijazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here