Home KITAIFA AHMED ALLY: TULIOWATANGAZA HAWAJATOSHA, BADO VYUMA VINAKUJA

AHMED ALLY: TULIOWATANGAZA HAWAJATOSHA, BADO VYUMA VINAKUJA

161
0

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba , Ahmed Ally, amesema wachezaji ambao itawatangaza si kama inamalizia zoezi la usajili, la hasha, bali imeshafanya hivyo na imeshapata vibali pamoja na Hati za Uhamisho wa Kimataifa, ITC.

“Hawa tuliowatangaza ambao kila mmoja anawafahamu hawajatosha bado kuna vyuma vitatu hatujavitambulisha, safari hii hatutaki mchezo,” alisema Ahmed.

Alisema wameshamaliza usajili wa wachezaji wote wa kigeni kwani mwisho wa usajili kwa nyota hao ilikuwa ni Agosti 15, mwaka huu.

Advertisement

“Tumemaliza usajili wa wachezaji wote wa kimataifa, tumepata vibali vyao pamoja na ITC zao na tayari dirisha la usajili la wachezaji wa nje ya nchi limeshafungwa tangu Agosti 15.

Hata wale ambao bado hatujawatangaza nao tumeshamaliza vibali na ITC zao ina maana ni wachezaji halali wa Simba tunasubiri wakati tu tulioupanga ili tuwatambulishe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here