Home KITAIFA HAJI MANARA AWAVAA WAKENYA KISA KEJERI ZAO KWA STARS

HAJI MANARA AWAVAA WAKENYA KISA KEJERI ZAO KWA STARS

86
0

Mdau maarufu wa mchezo wa mpira wa miguu Nchini Haji Manara amewajibu waandishi wa habari wa Kenya waliosema Taifa Stars wameumaliza mwendo kwenye mashindano ya CHAN baada ya kupangwa na Morocco.

“Kwani Sisi Tanzania ni Majirani wa Kenya au Watani zetu ? Au Siku hizi ni Mahasimu wa jadi? Na nani kawaambia wao tayari washafuzu kwa nusu fainali ?

“Halaf hii lugha ya kusema ngoja niongee kwa kiswahili ni dharau kuonyesha Wabongo hatujui kingereza. Aliowaambia Englisha ndio Alfa na Omega nani? Pls Acheni hayo mambo ndugu zetu, Sisi ni Wamoja na ni mipaka ya kikoloni iliyotufanya tuwe Mataifa mawili tofauti!!”.

Advertisement

“Ok,Tutawapasua Morocco Ijumaa hii na kuanzia leo ntatumia nguvu kubwa kuhamasisha tukaujaze Uwanja wa Mkapa ambao ndio Baba la Viwanja Afrika Mashariki”.Ameandika Haji Manara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here