KITAIFA TETESI ZA SOKA

MWAMBA HUYU WA KAZI KUSAINI YANGA SC

INAELEZWA kuwa Celestin Ecua ambaye ni kiungo wa Zoman FC huenda akasaini mkataba wa miaka miwili kuwa katika kikosi cha mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.

Yanga SC baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 walikusanya jumla ya pointi 82 ikiwaacha watani zao wa jadi Simba SC kwa tofauti ya pointi nne.

Simba SC iligotea nafasi ya pili ikiwa na pointi 78. Mchezo wa Kariakoo Dabi, Juni 25 2025 uliamua bingwa wa msimu baada ya Yanga SC kushinda kwa mabao 2-0 yakifungwa na Pacome kwa pigo la penalti na Clemet Mzize ambaye alitumia pasi ya Pacome.

Inaelezwa kuwa Ecua hueanda msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya Yanga SC akivaa uzi wa njano na kijani kwenye majukumu katika ligi namba nne kwa ubora.

Leave a Comment