KITAIFA

CHAN KUWAPA WACHEZAJI AZAM FC

AZAM FC matajiri wa Dar wamepanga kutumia michuano ya Kimataifa Afrika (Chan) kwa ajili ya kufanya usajili wa msimu ujao wa 2025/26.

Ipo wazi kwamba CHAN mchezo wake wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 2 kati ya Tanzania ambao ni wenyeji itakuwa dhidi ya Burkina Faso.

Tayari Azam FC imekamilisha usajili wa kipa mzawa Aishi Manula ambaye alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC amerejea kwa mara nyingin ndani ya kikosi hicho kwa changamoto mpya 2025/26.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Azam, Thabit Zakaria amesema kuwa wamepanga kusajili wachezaji wa kigeni wenye uzoefu wa kimataifa wakati wakijiandaa na Kombe la Shirikisho Afrika.

“Hatutaki kukurupuka katika usajili wetu, hivyo tutazingatia uzoefu wa wachezaji wa kucheza michuano ya kimataifa, hivyo tutatumia Chan kufanya skauti, “amesema Zakaria.

Leave a Comment