KITAIFA

YANGA SC YAZITAKA TATU ZA TANZANIA PRISONS

KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi amesema kuelekea kwenye mchezo wao wa mzunguko wa pili dhidi ya Tanzania Prisons msimu wa 2024/25 ambacho wanahitaji ni pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.

Yanga SC itakaribishwa na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Juni 18 2025 saa 10:00 ikiwa ni mzunguko wa pili.

Miloud amesema:”Tunawaheshimu sana Tanzania Prisons, lakini sisi ni Yanga. Nina wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini hatuna sababu ya kuwaza sana kuhusu hilo. Tumekuja kushindana kwa tahadhari kubwa na ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu.”

“Tumekuja Mbeya kusaka alama tatu tunawashukuru sana mashabiki, nimefanya kazi Klabu mbalimbali kubwa lakini mashabiki wa Yanga ni mashabiki wa mfano. Naamini kesho kwa mchango wao Uwanjani basi tutakuwa na wakati mzuri. Niwaombe sana mashabiki wajitokeze kwa wingi”

Kwenye msimamo Yanga SC ni nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 73 baada ya mechi 27 inakutana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 13 na pointi 30 baada ya mechi 28.

Leave a Comment