TETESI ZA SOKA

GIFT FRED: BEKI WA YANGA APATA DILI NONO

BEKI wa zamani wa Yanga SC Gift Fred ambaye alishindwa kupata namba kikosi cha kwanza na kupewa Thank You anatajwa kupata dili nono kwa ajili ya changamoto mpya.

Gift Fred anakaribia kujiunga na Klabu ya KCCA ya nchini Uganda katika msimu ujao wa 2025/26 kwa ajili ya kutimiza majukumu yake.

Gift anakwenda kujiunga na KCCA akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mkopo St George ya nchini Ethiopia kumalizika.

Ni Yanga SC ya Tanzania ilimpeleka beki huyo kwa mkopo St George  baada ya kutovutiwa na kiwango chake akishindwa kuwapa ushindani Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

Gift alitambulishwa ndani ya Yanga SC Julai 2023 alikwama kuonyesha uwezo katika mechi za ushindani.

Kwa sasa kwenye eneo la beki wa kati chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga SC ni Dickson Job ambaye huyu anatajwa kuwa ataongezewa kandarasi nyingine kubaki ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

Leave a Comment