Klabu ya Simba inaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na kiungo mshambuliaji wa klabu ya Mamelodi Sundowns Neo Maema ili kupata huduma yake kwa mkopo kuanzia msimu ujao.
Taarifa kutoka kwa mwandishi mkubwa wa michezo wa Afrika Kusini ni kuwa viongozi wa Simba tayari wameanza mazungumzo na Maema ambaye msimu uliopita amekuwa akikosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Mamelodi.
Maema mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Masandawana mwaka 2021 akitokea Bloemfontein Celtic amecheza michezo 120 na kufunga magoli 13 na kutoa pasi 14 za magoli.