Gwiji wa mchezo wa mieleka Duniani raia wa Marekani Terry Gene Bollea maarufu Hulk Hogan amefariki dunia siku ya leo kiwa nyumbani kwake Florida Nchini Marekani baada ya kupata mshuituko wa moyo.
Shirika kubwa la Mieleka Duniani WWE limethibitisha taarifa ya kifo cha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 71 na kumwelezea kama sura ya zama za dhahabu katika mieleka aliyekuwa na mchango mkubwa na usiofutika katika tasnia hiyo.