KITAIFA

AHMED ALLY ATHIBITISHA BALLA CONTE LIKUWA KWENYE MIPANGO YA FADLU

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwatuliza mashabiki wa Simba huku akithibitisha kuwa ni kweli kiungo Moussa Balla Conte aliyetambulishwa na wapinzani wao usiku wa leo alikuwa kwenye orodha ya kocha Fadlu.

“Wana Simba hakuna sababu ya kujisikia unyonge na wala tusijitie presha.Hii sio hadithi ya sizitaki mbichi hizi bali uhalisia wa jambo lenyewe.
tetesi za usajili simba 2025/26

“Iko hivi kwenye ripoti za Makocha hua kuna orodha ya majina mengi ya Wachezaji wanaopendekezwa
Ni kweli jina la mchezaji huyo lilikuwa kwenye orodha ya Kocha wetu kama yalivyokua majina mengine mengi Afrika nzima

“Wakati tunashiriki mashindano ya kimataifa kila mchezaji mzuri Mwalimu aliorodhesha jina lake na baadae kuyapanga kulingana na ubora wa mchezaji husika.

“Bahati mbaya au nzuri katika majina yote pendekezwa jina la mchezaji huyu ndio limekua maarufu baada ya kuzungumzwa sana kwenye mitandao.

“Umaarufu huo ukapelekea interest ya vyombo vya habari, na kuteka hisia za mashabiki.

“Lakini kiufundi hakuna tulichopoteza kwa sababu kweye orodha yetu wapo wachezaji bora sana kwenye eneo hilo tena waliopendekezwa na Mwalimu mwenyewe ambao ni chaguo la kwanza la pili na la tatu

“Tusitetereke ngome yetu ya usajili haijatikiswa hata kidogo
Muda wa utambulisho mtanielewa na kazi watakazofanya mtafurahi na mtakubali”.Ameandika Ahmed Ally.

Leave a Comment